Unguja,Zanzibar.
Huna pasipoti ya Mzanzibar,huchezi timu ya taifa ya Zanzibar,hii ni kwa mujibu wa shirikisho la soka visiwani Zanzibar,ZFA.
Shirikisho la soka visiwani Zanzibar,ZFA jana Jumapili kupitia kwa Afisa habari wake Cheupe limesema kuwa wachezaji watakaoitwa kuichezea timu ya taifa,Zanzibar Heroes ni wale tu ambao pasipoti zao zimezotolewa visiwani humo na siyo vinginevyo.
Kauli hiyo ya ZFA imekuja zikiwa ni siku kumi (10) tu zimepita tangu Zanzibar ikubaliwe kuwa mwanachama wa shirikisho la vyama vya soka Afrika,CAF.
Hii ina maana kwamba wachezaji wote ambao ni wazaliwa wa Zanzibar lakini pasipoti zao wamezipatia Tanzania bara hawataruhusiwa kuichezea Zanzibar Heroes.
0 comments:
Post a Comment