Paul Manjale
MCHEZO
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kati ya wenyeji Mbao FC na Simba SC
uliokuwa uchezwe Aprili 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza umesogezwa
mbele kwa siku mbili zaidi na sasa utachezwa Aprili, 10.
Taarifa iliyotolewa jioni ya leo na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura imesema mchezo huo umesogezwa mbele ili kupisha shughuli za kijamii zitakazofanyika kwenye uwanja huo kuanzia Aprili 1 mpaka Aprili 9.
0 comments:
Post a Comment