São Paulo,Brazil.
NEYMAR JR pichani akishangilia baada ya kuifungia Brazil bao moja katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Paraguay katika mchezo wa kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi.
Bao hilo la dakika ya 64 limemfanya Neymar Jr afikishe mabao 52 la kimataifa akiwa na jezi ya Brazil.Kabla ya bao hilo alikosa penati baada ya mkwaju wake kudakwa na kipa wa Paraguay, Antony Silva.
Mabao mengine ya Brazil yamefungwa na kiungo Philippe Coutinho katika dakika ya 35 pamoja na beki wa kushoto,Marcelo katika dakika ya 86 ya mchezo.
0 comments:
Post a Comment