Lameck Francis.
(Unguja,Zanzibar)
Katika kuhakikisha Zanzibar
inakuwa na mikakati thabiti kuhakikisha mpira unachezwa tofauti na mwanzo
ambapo Zanzibar haikuwa na uwanachama katika shirikisho la mpira barani afrika,CAF ,Kamati
Tendaji ya Chama cha Soka Visiwani Zanzibar “ZFA” leo imemchagua rasmi
kocha Abdulghany Msoma kuwa Mkurugenzi wa Ufundi “Technical Director” katika
kikao ambacho kimefanyika kwenye Ukumbi wa Magereza uliopo Kilimani Mjini
Unguja.
Akizungumza mara baada
ya kumalizika mkutano huo Afisa habari wa ZFA Ali Bakari “Cheupe” amesema
kamati tendaji ya ZFA wamemchagua Msoma kuwa Mkurugenzi wa Ufundi baada ya
kuona kuwa anastahili nafsi hiyo hivyo anaweza kuitendea haki kwa kipindi hiki
ambacho ligi kuu ya Zanzibar inatakiwa kubadilika kwa kufuata katiba mpya
walipewa na Caf
Msoma baada ya
kupatiwa nafasi hiyo amefurahishwa sana lakini kahimiza ushirikiano kati ya ZFA
na wadau wengine ili kuinua soka la Zanzibar kwani linahitaji nguvu kubwa ili
ligi iwe na mvuto na ushindani mkubwa kama zilivyo ligi nyingine.
0 comments:
Post a Comment