728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 29, 2017

    Yanga SC:Bado hatujaamua mchezo wetu dhidi ya MC Alger utachezwa wapi


    Paul Manjale.
    Dar Es Salaam,Tanzania.

    WAKATI kukiwa na taarifa kuwa huenda ikachezea mchezo wake wa kwanza wa hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria kwenye uwanja wa CCM Kirumba,Mwanza,Yanga SC kupitia kwa mjumbe wake wa kamati ya Utendaji,Salum Mkemi imesema bado haijaamua mchezo huo utachezwa kwenye uwanja gani.

    Akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio jijini hapa,Mkemi amesema wao kama uongozi bado hawajaamua ni wapi mchezo huo utachezwa.

    Mkemi ameongeza kuwa mchezo huo unaweza kuchezwa Uwanja wa Taifa ,Dar Es Salaam ama kokote kule nchini kwani Yanga SC ni timu ya Watanzania wote.Lakini amedokeza kuwa wazo la kuchezea mchezi huo CCM Kirumba limeukonga zaidi moyo wake.

    Yanga SC na MC Alger zinatarajiwa kuvaana Jumapili Aprili 8,kwenye mchezo wao wa kwanza wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika.Zitarudiana Aprili 16/17 huko Algers,Algeria.

    Wakati huohuo shirikisho la vyama vya soka Afrika,CAF jana Jumannne lilimtuma mkaguzi wake Maxwell Mtonga kutoka Malawi kwenda jijini Mwanza kwenda kuukagua uwanja wa CCM Kirumba ili kuona kama una hadhi ya kuchezewa michezo ya kimataifa ambapo licha ya dosari kadhaa kujitokeza, uwanja huo umeonekana kukidhi vigezo vingi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC:Bado hatujaamua mchezo wetu dhidi ya MC Alger utachezwa wapi Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top