London,England.
CHAMA cha soka cha Nigeria (NFF) kupitia kwa rais wake,Amaju Pinnick,kimemwonya staa wa nchi hiyo Victor Moses kuacha kuiletea pozi timu yake ya taifa,Super Eagles kwani kufanya hivyo kunaweza kumnyima nafasi ya kutwaa tuzo mchezaji bora wa mwaka wa Afrika.
Onyo hilo limetolewa baada ya hivi karibuni Moses,26, kujitoa kwenye kikosi cha Nigeria ambacho leo hii kitacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Senegal huko London kwa madai ya kuwa majeruhi.
Licha ya Moses kufika kwenye kambi ya Nigeria iliyoko kwenye hoteli ya Crowne Plaza iliyoko jijini London kuuthibitisha kuwa hasingizii majeruhi lakini kukosekana kwake kikosini kumeripotiwa kumelisononesha sana benchi zima la ufundi la timu hiyo linaloongozwa na Mjerumani,Gernot Rohr.
Hii ni mara ya pili kwa Moses kujiondoa kwenye kikosi cha Nigeria kwa madai ya kuwa majeruhi.Mara ya kwanza ilikuwa ni mwezi Novemba mwaka jana pale alipoukosa mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 dhidi ya Zambia.
Akifanya mahojiano na gazeti la The Guardian,Raisi wa cha soka cha Nigeria,Amaju Pinnick amesema Moses anapaswa kufahamu kuwa kwa kiwango chake bora anachoendelea kukionyesha akiwa na timu yake ya Chelsea anajiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Afrika hasa kama timu hiyo itatwaa ubingwa wa ligi kuu England msimu huu.
Pinnick ameongeza kuwa jambo hilo linaweza kutimia tu ikiwa Moses atakuwa akicheza mara kwa kwenye kikosi cha Nigeria na kuacha kukwepa kwepa mialiko ya makocha wake.
0 comments:
Post a Comment