Faridi Miraji , Dar es salaam.
Timu ya Taifa ya vijana nchini Tanzania , Serengeti boys imeifunga wenzao wa timu ya Taifa ya Burundi kwenye mchezo wa kirafiki iliofanyika uwanja wa Kaitaba , mkoni Kagera na kushuhudia Serengeti boys ikishinda kwa magoli matatu bila majibu
Magoli ya Serengeti boys yamewekwa kimiyani na Muhisin Makame dakika ya 20 na goli la pili la Serengeti boys limefungwa na beki wa kushoto Niksoni Kibabage dakika ya 39 huku goli la mwisho likiwekwa kambani na mshambuliaji tegemezi wa timu ya Taifa Yohana Nkomola dakika ya 72 kwa mkwaju wa penalty.
Serengeti boys mwendo ni Gabon mpaka kombe la Dunia
0 comments:
Post a Comment