728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 22, 2017

    Mchezaji auwawa na mamba akiwa mazoezini


    Maputo,Msumbiji.

    MCHEZAJI kinda wa klabu ya Atletico Mineiro de Tete inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Msumbiji,Estevao Alberto Gino ameuwawa baada ya kushambuliwa na mamba akiwa mazoezini kanda kando ya Mto Zambezi.

    Gino,19,amekumbwa na umauti huo Alhamisi iliyopita huko Magharibi wa jimbo la Tete.Taarifa rasmi imetoka jana Jumanne.

    Mashuhuda wa tukio hilo wamesema baada ya kumaliza kufanya mazoezi kando ya mto huo,Gino alijongea majini kupoza mwili wake na hapo ndipo aliponaswa na mamba huyo anayedaiwa kuwa na urefu wa mita tano na kukimbia nae.Amesema kocha na mmiliki wa klabu ya Atletico Mineiro de Tete,Eduardo Carvalho akiwanukuu watu wawili walioshuhudia tukio hilo.

    Msemaji wa jeshi la polisi wa jimbo la Tete,Leonel Muchina,amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mpaka sasa mwili wa mchezaji huyo bado haujapatikana.

    Matukio ya watu kuuwawa na mamba kando ya mto Zambezi yamekuwa hadithi isiyokwisha kwani mto huo umeripotiwa kuwa na mamba wengi kuliko kawaida huku ukiwa tegemeo kuu la wakazi wa maeneneo ya jirani ambao huutegemea mto huo kupata maji ya kunywa.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mchezaji auwawa na mamba akiwa mazoezini Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top