728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 24, 2017

    Viwango vya ubora wa soka la wanawake duniani:Tanzania kinara Afrika Mashariki,Ujerumani ya kwanza kidunia


    Geneva,Uswisi.

    TIMU ya taifa ya soka ya wanawake ya Tanzania,Twiga Stars imeshika nafasi ya 106 kidunia na nafasi ya kwanza Afrika Mashariki kwenye orodha ya ubora wa viwango vya soka la wanawake iliyotolewa leo hii na shirikisho la soka duniani,FIFA.

    Twiga Stars imeshika nafasi ya kwanza Afrika Mashariki na ya 106 kidunia baada ya kujikusanyia pointi 960.Nafasi ya pili imechukuliwa na Rwanda huku kidunia ikiwa nafasi ya 108.Imejipatia pointi 908.

    Nafasi ya tatu imechukuliwa na Kenya,kidunia imeshika nafasi ya 110.Imejikusanyia pointi 857.Uganda ni ya nne,kidunia ni ya 112. Imejikusanyia pointi 836.

    Afrika,Nigeria imeshika nafasi ya kwanza,kidunia nafasi ya 34.Ghana imeshika nafasi ya pili Afrika,kidunia nafasi ya 45.Nafasi ya tatu imeshikwa na Cameroon, kidunia nafasi ya 47.

    Kidunia,Ujerumani imeshika nafasi ya kwanza ikiiondoka Marekani katika nafasi hiyo kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2015.Nafasi ya pili imeshikwa na Marekani,Ufaransa iko nafasi ya tatu.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Viwango vya ubora wa soka la wanawake duniani:Tanzania kinara Afrika Mashariki,Ujerumani ya kwanza kidunia Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top