728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, March 27, 2017

    Uholanzi yatimua kocha


    Paul Manjale

    Amsterdam, Uholanzi.

    UHOLANZI imetangaza kumtimua kazi aliyekuwa kocha wake mkuu Danny Blind,baba mzazi wa kiungo wa Manchester United,Daley Blind.

    Taarifa iliyotolewa na chama cha soka cha Uholanzi (KNVB) imesema kutimuliwa kwa Blind aliyehudumu kwa miezi 20 kunatokana na muendelezo wa matokeo mabovu inayoendelea kuipata timu hiyo ya taifa.

    Blind alijulishwa kuhusu kutimuliwa kwake jana Jumapili katika kikao chake na wakurugenzi wa michezo na ufundi Jean Paul Decossaux na Hans van Breukelen.


    Ikumbukwe juzi Jumamosi Uholanzi ilichapwa mabao 2-0 na Bulgaria katika mchezo wa kundi A wa kuwania tiketi ya kufuzu kombe la dunia.Kichapo hicho kimeiacha Uholanzi ikiwa nafasi ya nne,pointi tano nyuma ya vinara Ufaransa na pointi tatu nyuma ya Sweden anaoshikilia nafasi ya pili.

    Blind alianza kuifundisha Uholanzi Julai 2015 akichukua nafasi ya Guus Hiddink aliyejiuzulu baada ya kuona mambo hayaendi sawa.

    Kocha wa kikosi cha U-20 Fred Grim amepewa mikoba ya kuwa kocha mkuu wa muda katika kipindi hiki ambacho KNVB ipo katika mawindo ya kumsaka kocha mpya.Uholanzi itashuka tena dimbani Jumanne hii kucheza na Italia katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Uholanzi yatimua kocha Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top