Brasilia,Brazil.
STAA wa Brazil na Barcelona,Neymar Jr amesema hana mpango wala nia ya kushindana na wakali kama Cristiano Ronaldo na Lionel Messi kwenye kinyang'anyiro cha kumsaka mchezaji bora wa mwaka wa dunia.
Neymar Jr mwenye umri wa miaka 25,amewaambia waandishi habari wa nchini kwao Brazil kuelekea mchezo wao wa leo usiku wa kuwania tiketi ya kufuzu fainali za kombe la dunia dhidi ya Paraguay,kuwa hafikirii kabisa kuwafikia ama kuwafunika wakali hao.Mchezaji pekee anayefikiria kumfikia na ikibidi kumfunika kabisa ni yeye mwenyewe yaani Neymar Jr.
Neymar ameongeza kama kuna kitu kinachomkera na hakipendi basi ni kushindanishwa na wakali hao ambao katika miaka kumi iliyopita wamekuwa wakipokezana kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa dunia maarufu kama Ballon d’Or.
Wakati huohuo Neymar Jr amekiri kuwa Messi na Ronaldo ni wachezaji wakali sana.Anawahusudu na amekuwa akijifunza mambo mengi sana kutoka kwao.
0 comments:
Post a Comment