Dortmund,England.
Lukas Podolski (Pichani) akishangilia bao lake la umbali wa mita 30 aliloifungia Ujerumani na kuiwezesha kuifumua England bao 1-0 kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa Jumatano usiku huko Signal Iduna Park jijini Dortmund.
Podolski aliyekuwa akichezea Ujerumani mchezo wake wa mwisho wa kimataifa baada ya kuamua kutundika daruga alifunga bao hilo katika dakika ya 69 baada ya kufumua mkwaju mkali wa mguu wa kushoto uliomshinda kipa wa England,Joe Hart na kutinga wavuni.Pasi ikitoka kwa Andre Schurrle.
Podolski,31, anaiacha Ujerumani baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 15 akiichezea michezo 130 na kuifungia mabao 49.Pia aliisaidia kutwaa kombe la dunia la mwaka 2014 nchini Brazil.
Mapema kipindi cha kwanza Adam Lallana alishindwa kuifungia bao la kuongoza England baada ya mkwaju wake kugonga mwamba wa lango la Ujerumani lililokuwa chini ya mlinda mlango wa Barcelona, Marc Ander Stergen.
0 comments:
Post a Comment