728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 25, 2017

    Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya Jumamosi ya leo Machi 25,2017

    Leon Goretzka

    Paul Manjale.

    Mbappe:Monaco imekataa dau la £96m (€110m) ambalo lingeweka rekodi ya kuwa dau kubwa zaidi la usajili wa wachezaji duniani kutoka timu moja ya England kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake kinda,Kylian Mbappe,18.(AS)

    Alonso:Kiungo wa Bayern Munich,Xabi Alonso,35, amefichua kwamba alikaribia kujiunga na Arsenal mwaka 2009 lakini klabu hiyo ya Emirates ilikataa kuongeza £3m tu ili kufikia dau la £18m lililokuwa likitakiwa na Liverpool.(Liverpool Echo)

    Silva:Bayern Munich inafikiria kutoa kitita cha €80m kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Monaco,Mreno Bernardo Silva. Bayern Munich inamwona Silva,22, kama mrithi wa muda mrefu wa viungo wake Philipp Lahm na Xabi Alonso ambao watastaafu mwisho wa msimu huu.(A Bola).

    Goretzka:Arsenal imeripotiwa kuwa itapambana na Tottenham kujaribu kumsajili kiungo wa Schalke,Leon Goretzka.Goretzka,22, amekataa mkataba mpya wa kuendelea kusalia Schalke na klabu hiyo ya Ujerumani imeripotiwa kuwa tayari kumuuza nyota huyo mwishoni mwa msimu huu. (Daily Mirror)

    Belotti:Arsenal imetuma ofa ya €52.1m (£43.2m) kwenda Torino kwa ajili ya kuangalia uwezekano wa kumsajili mshambumbuliaji wake hatari,Andrea Belotti mwenye mabao 22 msimu huu.Mbali ya Arsenal,Napoli nayo imeripotiwa kutuma ofa kama hiyo pamoja na kuwa tayari kumtoa mshambuliaji wake,Leonardo Pavoletti.Belloti anadaiwa kuwa na thamani ya €100m (£86.5m).(Tuttosport)

    Xhaka:Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka amesema bado ana furaha kuendelea kucheza Emirates na hana habari kama Bayern Munich inamtaka.(London Evening Standard)

    Coutinho:Kiungo wa zamani wa Hispania,Luis Garcia amemtaka kiungo wa Brazil,Philippe Coutinho kutoihama Liverpool hivi karibuni licha ya kuwindwa kwa nguvu zote na Barcelona.(Liverpool Echo )

    Carole:Crystal Palace imeripotiwa kuwa itajaribu kwa mara nyingine tena kumsajili mlinzi wa Galatasaray,Lionel Carole baada ya kumkosa msimu uliopita.(Croydon Advertiser )

    Benzema:Rais wa Real Madrid,Florentino Perez amemtaka mshambuliaji wake Karim Benzema kuendelea kubaki klabuni hapo kwa miaka mingi zaidi.Benzema alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 akitokea Lyon.(Radio Montecarlo)

    Kolasinac:Manchester City imeanza mazungumzo na wakala wa mlinzi wa kushoto wa Schalke,Sead Kolasinac kwa ajili ya kumsajili mteja wake mwishoni mwa msimu huu.Kolasinac,25,amebakiza miezi michache kumaliza mkataba wake Schalke.(Bild)

    Djourou:West Ham mlinzi wa zamani wa Arsenal,Johan Djourou,ambaye atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu.Kwa sasa Djourou,30, anaichezea Hamburg ya Ujerumani. (The Sun).



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Hizi hapa habari kubwa za usajili kutoka barani Ulaya Jumamosi ya leo Machi 25,2017 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top