Machakos,Kenya.
WAPINZANI wakubwa wa soka la ukanda wa nchi za Afrika Mashariki,Kenya na Uganda leo jioni wameshindwa kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo mkali wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa kumbumbuku ya Jomo Kenyatta huko Machakos.
Katika mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji wengi ilishuhudiwa Kenya ikijipatia bao lake katika dakika ya 35 kupitia kwa mshambuliaji wake mrefu ,Michael Olunga "Engineer"
huku Uganda wao wakijipatia bao lao katika dakika ya 87 ya mchezo kupitia kwa kinda wake Moses Waiswa aliyekuwa akicheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa.
Kenya wanapaswa kujilaumu kwa kushindwa kupata ushindi katika mchezo huo kwani waliimudu vyema Uganda lakini washambuliaji wake wakiongozwa na Michael Olunga walishindwa kuzitumia nafasi nyingi za mabao zilizopatikana.
Kocha wa Kenya,Stanley Okumbi alikifanyia mabadiliko makubwa kikosi chake jioni ya leo kwa kuwaweka benchi nyota wake mahiri kama nahodha Victor Wanyama,David ‘Calabar’ Owino na David ‘Cheche’ Ochieng na kuwapa nafasi nyota wapya kama Patrick Matasi,Robinson Kamura na Sammy Onyango.
Kocha wa Uganda,Milutin ‘Micho’ Sredojevic aliwajumuisha kikosini nyota kama Shafik Batambuze,Godfrey Walusimbi,Murshid Juuko,Emanuel Okwi na nahodha Hassan Wasswa.
0 comments:
Post a Comment