Unguja.
CHAMA cha soka cha Zanzibar,ZFA kimetangaza kuondoa zawadi ya mpira kwa mchezaji atayefunga mabao matatu ( Hat-trick) dhidi ya klabu ya Kimbuka FC inayoshiriki ligi kuu ya visiwani humo.
Akitoa taarifa hiyo msemaji wa ZFA,Ally Bakari Cheupe amesema wameamua kuchukua uwamuzi huo baada ya Kimbuka FC kushindwa kuonyesha upinzani wowote kwenye ligi hiyo na badala yake kuonekana ipo tu kwa ajili ya kukamilisha ratiba na siyo kushindana.
Tangu kuanza kwa ligi kuu Zanzibar Octoba 27 mwaka jana,Kimbuka FC iliyoko kanda ya Unguja imekuwa ikiburuza mkia kwani mpaka sasa imecheza michezo 27 na kuambulia pointi 5 pekee.
0 comments:
Post a Comment