728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 25, 2017

    Samatta apiga mbili,Stars ikiiadhibu Botswana 2-0 U/Taifa


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    TAIFA STARS imerejesha tabasamu kwa mara nyingine kwenye sura za mashabiki wake baada ya jioni ya leo kuifunga Botswana kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

    Mabao yote mawili ya mchezo huo ulioshuhudiwa na mashabiki wengi kiasi yametiwa kimiani na nahodha,Mbwana Ally Samatta katika dakika ya 3 na 87.

    Samatta alifunga bao la kwanza baada ya kuwaponyoka mabeki wa Botswana kisha akafunga bao la pili kwa mkwaju wa faulo uliopatikana baada ya yeye wenyewe kufanyiwa madhambi.

    Taifa Stars itarejea tena dimbani katikati ya wiki ijayo kucheza mchezo wake wa pili wa kirafiki kwa kuvaana na Burundi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Samatta apiga mbili,Stars ikiiadhibu Botswana 2-0 U/Taifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top