728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 30, 2017

    Claudio Tapia bosi mpya chama cha soka Argentina


    Paul Manjale.

    CLAUDIO Chiqui Tapia ndiye Raisi mpya wa chama cha soka cha Argentina,AFA hii ni baada ya kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika jana Jumatano huko Buenois Aires,Argentina.

    Tapia,49,aliyekuwa mgombea pekee kwenye nafasi hiyo,ameshinda baada ya kupata kura 40 kati ya kura 43 zilizopigwa huku vilabu vya River Plate,Banfield na San Lorenzo vikiripotiwa kugoma kumpigia kura kwa madai ya kutomkubali.

    Kabla ya kuwa Raisi mpya wa AFA,Tapia alikuwa akihudumu kama Rais wa klabu ndogo ya Barracas Central inayoshiriki ligi daraja la tatu nchini Argentina,Primiera B.

    Kuchaguliwa kwa Tapia kunakuja kama neema kwa soka la Argentina ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa halina mwelekeo chanya hasa baada ya kufariki kwa aliyekuwa Raisi wake wa zamani,Julio Grondona hapo mwaka 2014.

    Kabla ya uchaguzi wa jana Jumatano,Argentina ilipitia mikononi mwa Maraisi wawili wa muda,Luis Segura na Armando Pérez.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Claudio Tapia bosi mpya chama cha soka Argentina Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top