728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 22, 2017

    Lehmann awataja watatu wanaoiangusha Gunners.


    Munich,Ujerumani.

    Golikipa wa zamani wa klabu ya Arsenal Jens Lehmann amesema kwamba Alexis Sanchez hawezi kuitwa mchezaji mkubwa kama akiendelea kununa nuna.

    Sanchez amekuwa akionesha huzuni yake kubwa mara kwa mara hasa katika kipindi hiki kigumu cha Gunners, kipindi ambacho Arsenal wameangukia mbali kwenye mbio za Ubingwa na kutolewa kwenye mashindano ya UEFA hatua ya 16 bora kwa mara ya saba mfululizo.

    Lehmann pia amehoji uimara wa Mjerumani mwenzake Mesut Ozil  ambaye amekuwa akikosolewa mara kwa mara kwa kushindwa kuonesha ubora wake pindi Arsenal wanapokabiliana na mechi ngumu dhidi ya Vilabu vikubwa.



    Lehmann ambaye amewahi kuwa Golikipa bora wa UEFA mara mbili pia hajaridhishwa na kiwango cha beki Shokdran Mustafi ambaye alijiunga na Arsenal kwa thamani ya pauni milioni 35 kutoka Valencia.

    "Wanaongea kuhusu Sanchez kuwa mchezaji mkubwa , lakini kama unanuna nuna huwezi kuwa mchezaji mkubwa."

    "Unatakiwa kuwa mchezaji mkubwa kwa uimara wa kiakili, sio tu mzuri kwenye kukokota mpira."

    "Siku zote kumekuwa na walakini kuhusu Ozil - ni kwa kiasi gani anaweza kuchangia pindi mambo yakiwa magumu .? "

    "Sio kosa la Mustafi kwamba watu wamelipa pauni milioni 35 . kama mtu akilipa pauni milioni 35 kwa ajili yangu - Siku inayofuata sio mchezaji mzuri."

    "Anajituma sana, Lakini kama timu inaruhusu magoli matano, lazima ujiulize kama unazuia vya kutosha."

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Lehmann awataja watatu wanaoiangusha Gunners. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top