London,England.
West Ham wameonesha nia ya kutaka kumsajili Wayne Rooney kama Manchester United watamruhusu kuondoka Old Trafford majira ya kiangazi kwa mujibu wa taarifa kutoka Sky sports.
Rooney ameanza mechi 9 tu za EPL tangu Jose Mourinho alipo kabidhiwa mikoba ya kuinoa Man United mwezi Juni mwaka jana.
Mkataba wake unafikia tamati mwaka 2019 , lakini United wanatarajiwa kumruhusu mwishoni mwa msimu huu.
Chanzo cha Habari kutoka West Ham kimethibitisha kwamba West Ham watakuwa moja ya vilabu vitakavyowania saini ya Wazza kama United wakionesha dalili ya kumruhusu nyota huyo.
United walimsajili Rooney kutoka Everton kwa pauni milioni 27 mwaka 2004 . Tangu kipindi hiko ametwaa mataji matano ya EPL na Moja la UEFA mwaka 2008.
Amekuwa mfungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akiwa ameweka kambani mara 250 .
Rooney aliwahi kusema kwamba klabu ambayo anaweza kuitumikia baada ya kuondoka United katika ligi kuu ya Uingereza ni Everton pekee.
0 comments:
Post a Comment