728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Wazee wa Vipepsi kuongezewa adhabu zaidi England


    London, England.

    CHAMA cha soka nchini England,FA kinafikiria kuwaongezea adhabu zaidi wachezaji wenye tabia za kihuni za kuwachapa wachezaji wenzao viwiko/vipesi wawapo viwanjani.

    FA imefikia hatua hiyo baada ya hivi karibuni matukio hayo kuendelea kushika kasi badala ya kupungua licha ya adhabu yake kuwa ni kifungo cha kukosa michezo mitatu.

    FA inaona adhabu hiyo imekuwa siyo tishio tena kwa wachezaji hivyo inafikiria kuiongezea makali zaidi ili kukomesha matukio hayo ambayo yamekuwa yakiupaka matope mchezo wa soka.

    Hivi karibuni mshambuliaji wa Rochdale,Calvin Andrew alilimwa adhabu kali ya mfano baada ya kufungiwa michezo 12 kwa kosa la kumchapa kiwiko kizito mchezaji wa Oldham,Peter Clarke.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wazee wa Vipepsi kuongezewa adhabu zaidi England Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top