Paul Manjale.
STAA wa zamani wa Brazil na mshindi mara mbili wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia,Ronaldinho amegeukia fani ya muziki baada ya jana Jumanne kupakua kibao chake cha kwanza ambacho amekiita SOZINHO akimaanisha Alone ama Pekee kwa lugha ya kiswahili.
Kibao hicho ambacho kina urefu wa dakika 4:15 kimeimbwa katika mahadhi ya muziki wa Samba ambao ni maarufu sana nchini Brazil.
Akiutambulisha wimbo huo,Ronaldinho amesema kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii "Asanteni marafiki zangu,huu ni wimbo wangu wa kwanza,nimeutunga mwenyewe"Alimaliza Ronaldinho ambaye amekuwa nje ya dimba tangu mwaka 2015.
0 comments:
Post a Comment