728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 30, 2017

    Ghana yathibitisha vijana wake wake wanatua nchini kesho Ijumaa kuivaa Serengeti Boys


    Accra,Ghana.

    CHAMA cha soka cha Ghana,GFA kimethibitisha kuwa timu yake ya taifa ya vijana waliochini ya umri wa miaka 17,Black Starlets itatua nchini Ijumaa ya wiki hii kucheza mchezo mmoja wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya  vijana ya Tanzania ya umri huo,Serengeti Boys.

    Mchezo huo utakaotumika kama sehemu ya maandalizi ya timu hizo mbili kabla ya kuelekea nchini Gabon kwenye fainali za michuano ya vijana wa umri huo umepangwa kufanyika Jumatatu ya Aprili 3 kwenye uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam.

    Baada ya mchezo huo Black Starlets itarejea nyumbani Ghana ambapo siku ya Jumapili,Aprili 16 itashuka kwenye dimba la Uwanja wa Accra kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya vijana ya Niger.

    Ghana imepangwa kundi A pamoja na nchi za Guinea Cameroon na wenyeji Gabon wakati Serengeti Boys yenyewe imepangwa kundi B.

    Michuano ya vijana itaanza kutimua vumbi lake Mei 14 huko nchini Gabon na timu zitakazomaliza katika nafasi nne za juu zitapata tiketi ya kuiwakilisha Afrika kwenye fainali za kombe la dunia la vijana litakalofanyika baadae mwaka huu nchini India.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ghana yathibitisha vijana wake wake wanatua nchini kesho Ijumaa kuivaa Serengeti Boys Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top