FaridMiraji,Dar Es Salaam.
Kuanzia mwaka 2026 kombe la Dunia litashirikisha timu 48 kutoka Mabara 6 ambazo zitagawanywa Makundi 16 yenye timu 3 ambazo kila timu itacheza mechi mbili na timu moja kila kundi itafuzu Hatua ya 16 Bora.
Hii Itakuwa tofauti na sasa ambayo ina timu 32 ambazo zipo makundi 8 yenye timu 4 kila kundi na kila timu hucheza mechi tatu na timu mbili za juu kufanikiwa kuingia Hatua ya 16 Bora.
ZINAPATIKANAJE 48
Mabara matano kati ya sita yaneongezewa timu kama ifutavyo Bara la Ulaya (UEFA) walikuwa na timu 13 sasa wameongezewa mpaka 16, Bara la Amerika kusini (CANMEBOL) walikuwa wanatoa timu 5 wameongezewa timu moja na sasa watatoa timu 6, Kwa Amerika Kaskazini. (CONCACAF) wao wameongezewa nafasi mbili kutoka 4 hadi sita, Bara Asia (AFC) walikuwa wanatoa timu 4 na sasa watatoa timu 8 , Huku Bara letu la Afrika(CAF) wakiongezewa nafasi 4 kutoka 5 hadi 9 ambazo watatakiwa kutoa kuanzia kombe la 2026. Bara la Oceania(OFC) lenyewe litatoa timu moja.
16+9+8+6+6+1=46 kwenye 48 Bado timu mbili Unajua wanazipataje ? Kutakuwepo na play off ya kupata timu mbili kuanzia kombe la dunia 2026. Pia Bara mwenyeji nafasi ya mwenyeji itakuwepo kwenye idadi husika Mfano kombe la dunia 2030 lichezwe Afrika. Africa watatakiwa kutoa timu 8 na moja watamwachia mwenyeji hivyo hivyo Kwa Mabara
Mengine. Play off itahusisha timu 5 kutoka Mabara matano isipokuwa ulaya ila ulaya akiwa mwenyeji wataruhusiwa kuingiza timu kwenye play off. Hizi zitacheza kupata timu mbili ambazo zitaungana na zile timu 46 kukamilisha idadi ya timu 48.
0 comments:
Post a Comment