James Eduma,Iringa.
Uongozi wa chama cha soka mkoani Iringa (IRFA) umekiri kutokuwepo
kwa mahusiano mazuri kati yao na viongozi wa klabu ya Lupuli FC ambao
wana jukumu la kuiwezesha timu yao kujiandaa vyema kabla ya kuanza kwa ligi kuu
ya soka Tanzania bara msimu wa 2017/18.
Katibu mkuu wa IRFA, Ally Ngallah ameelezea sintofahamu hiyo
iliyogubika miongoni mwa viongozi wa klabu hiyo kongwe hapa nchini, hadi
kufikia hatua ya kutokua na uhusiano mzuri na chama cha soka mkoa wa Iringa.
Hata hivyo Ngallah amesema uongozi wa IRFA unaendelea kupambana
ili kumaliza sintofahamu ya viongozi wa Lupuli FC ili kusaidia mchakato wa
kupatikana kwa mwenendo mzuri ambao utaisaidia klabu hiyo kufanya usajili wa
wachezaji vizuri pamoja na kuwa na maandalizi mazuri ya ligi kuu.
Katika hatua nyingine Ngallah amezungumzia uwanja wa Samora ambao
utatumiwa na klabu ya Lipuli FC katika michezo ya ligi kuu msimau ujao wa ligi,
kwa kusema upo katika hali nzuri na umekidhi vigezo.
Amesema uwanja huo umefanyiwa marekebisho ya hali juu baada ya
kupokea taarifa za maelekezo kutoka TFF.
0 comments:
Post a Comment