Gijon,Hispania.
Hispania na Italia zimeendelea kukabana koo kileleni mwa msimamo wa kundi G la kuwania kukata tiketi ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018, baada ya jana usiku zikiwa kwenye viwanja vyao vya nyumbani kupata ushindi mnono dhidi ya wageni wao Israel na Albania.
Hispania ikiwa nyumbani Estadio El Molinon jijini Gijon imeifumua Israel mabao 4-1.Shukrani kwa mabao ya David Silva, Vitolo, Diego Costa na Isco.Bao la Israel limefungwa na Lior Refaelov.
Katika mchezo mwingine, Italia ikiwa nyumbani Stadio Renzo Barbera imeiduwaza Albania kwa kuifunga mabao 2-0 ya Daniele Di Rossi aliyefunga kwa mkwaju wa penati na staa wa Lazio,Ciro Immobile.
Ushindi huo umefanya Hispania na Italia ziendelee kukabana koo kileleni baada ya zote kufikisha pointi 13 katika michezo mitano lakini Hispania inabebwa na uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
BOFYA HAPA KWA MATOKEO ZAIDI:http://www.bbc.com/sport/football/world-cup-qualifying-european/results
0 comments:
Post a Comment