728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 29, 2017

    Nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa Uganda Cranes aachana na soka la kimataifa


    Paul Manjale.

    NAHODHA na mfungaji bora wa muda wote wa timu ya taifa ya Uganda,Uganda Cranes,Godfrey Massa hataichezea tena timu hiyo hii ni baada ya leo mchana kutangaza kustaafu soka la kimataifa.

    Kustaafu kwa Massa kunakuja ikiwa ni miezi michache tu imepita tangu mshambuliaji huyo mwenye nguvu afanikiwe kuiongoza Uganda Cranes kufuzu michuano ya AFCON kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1978.

    Akifanya mahojiano na Daily New Vision,Massa,34, amesema ameamua kustaafu kuichezea Uganda Cranes baada ya kushauriana kwa muda mrefu na familia yake.Pia ameona kuwa huu ni muda sahihi kwake kujiweka pembeni na kuzipisha damu changa.

    Massa aliichezea Uganda Cranes kwa mara ya kwanza mwaka 2006 na mwaka 2015 alichaguliwa kuwa nahodha mkuu.

    Mpaka anastaafu leo,Massa ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa muda wote wa Uganda akiwa amepachika mabao 12.Kwa sasa Massa ni mchezaji huru baada ya mwezi Februari mwaka huu kutemwa na Baroka FC ya Afrika Kusini.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Nahodha na mfungaji bora wa muda wote wa Uganda Cranes aachana na soka la kimataifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top