Dar Es Salam,Tanzania.
TIMU za vijana za Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, chini ya umri wa miaka 11 (U-11) na 13 (U-13) inatarajia kushiriki michuano maalumu ya vijana nchini (JMK Mini Cup) itakakayofanyika kwenye Uwanja wa Kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete (JMK Park) Aprili Mosi mwaka huu kuanzia 2.30 asubuhi hadi saa 6.00 mchana.
Hiyo ni michuano ya kwanza kwa timu hizo kushiriki, tokea zilipoundwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa pamoja kikiwa na jumla ya wachezaji 29 wenye vipaji vya hali ya juu na baadhi ambao wanahitaji kujengwa vema.
Michuano hiyo inatarajia kushirikisha jumla ya timu nne za vijana zitakazoleta timu zao za vijana chini ya umri wa miaka 10 na 13, ambazo ni Azam FC, Dar es Salaam Football Academy (D.FA), timu ya Shule ya Kimataifa ya Tanganyika (IST) na wenyeji JMK Park.
Akizungumza na mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz Mkuu wa Maendeleo ya Soka la Vijana Azam FC, Tom Legg, alisema michuano hiyo itawapa nafasi vijana kushindana wenyewe kupitia mechi huku akikutana na changamoto ya presha kwenye mechi za ushindani.
“Michuano ya JMK Mini Cup, itawapa nafasi vijana wangu kushindano wenyewe kupitia mechi ambazo zitakuwa na presha, msisitizo kutoka kwa makocha huwa ni kuangalia kwa umakini utendaji kazi wa wachezaji kuanzia mchezaji mmoja mmoja na kwa timu nzima.
“Lakini huwezi kuondoa presha ambayo hutokea wakati wa kucheza mechi ambayo malengo mafupi (ni kupata matokeo) ambayo huwa na athari katika malengo makubwa (kushinda kombe,” alisema Legg.
Vikosi hivyo vimekuwa katika programu ya kila wiki na kucheza mechi kila wikiendi, ambapo vimekuwa vikifanya mazoezi siku ya Jumanne, Alhamisi na Jumamosi kama zikiwa hazina mechi.
Azam FC kwa sasa upo katika mchakato wa kuunda upya timu zake za vijana kuanzia miaka 20, ambayo ipo hatua za mwishoni baada ya wachezaji mbalimbali walioonekana kwenye michuano ya vijana ya Ligi Kuu iliyomalizika mwishoni mwa mwaka jana kuchukuliwa kufanyiwa majaribio na kupatikana wale bora watakaounda timu bora wakiungana na baadhi waliobaki katika kikosi hicho kilichoshika namba mbili.
0 comments:
Post a Comment