London,England.
ARSENAL imeripotiwa kuwa itahitaji kupata malipo ya £50m kama ada ya uhamisho ya Alexis Sanchez ikiwa staa huyo wa Chile ataendelea kugomea kusaini mkataba mpya na kuamua kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Kwa mujibu habari kutoka gazeti la Uingereza la Evening Standard,Arsenal imeamua kutaja bei hiyo baada ya kuona kuwa kuna kila dalili kuwa imeshindwa vita ya kumshawishi staa huyo atulize akili yake na kusaini mkataba mpya Emirates.
Katika siku za hivi karibuni Sanchez,28,aliyebakiza mwaka mmoja mkwenye mkataba wake wa sasa ,amekuwa kwenye msuguano mkali na Arsenal hasa baada ya kuomba kuongezewa mshahara kutoka £150,000 kwa wiki mpaka £230,000 ndipo akubali kusaini mkataba mpya.Ombi ambalo limepigwa chini na Arsenal na kuibua hofu kuwa huenda staa huyo akatimkia Bayern Munich, Real Madrid ama Chelsea.
Sanchez alijiunga na Arsenal mwaka 2014 akitokea Barcelona kwa ada ya £34m.Msimu huu Sanchez ameifungia Arsenal mabao 22 na kupika/assist mabao18 katika michezo 38.
0 comments:
Post a Comment