728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 29, 2017

    Argentina bila Messi kumbe weupe tu,wanyukwa 2-0 na Bolivia kombe la dunia,Chile,Colombia zashinda


    Paul Manjale

    IKICHEZA bila ya nahodha wake,Lionel Messi aliyefungiwa michezo minne kwa kosa la kumtolea lugha ya matusi mwamuzi msaidizi/mshika kibendera,Marcelo Van Gasse Alhamisi iliyopita,Argentina imeonekana kuwa si lolote si chochote baada ya usiku wa kuamkia leo kuchabangwa mabao 2-0 na Bolivia katika mchezo mkali wa kuwania kukata tiketi ya kucheza michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 nchini Urusi kwa mataifa ya kanda ya Amerika Kusini,CONMEBOL.


    Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la uwanja wa Estadio Hernando Siles,ilishuhudia wenyeji Bolivia wakijipatia mabao yao katika dakika za 31 na 52 kupitia kwa Juan Carlos Arce na Marcelo Martins huku Argentina wakipata pigo baada ya beki wake wa kati Ramiro Funes Mori kulazimika kutolewa nje kwa msaada ya machela baada ya kupata jeraha baya la goti.

    Kichapo hicho kimeitupa Argentina nje ya nafasi nne za juu za kanda hiyo hasa baada ya Chile ikiwa nyumbani Estadio Monumental,Santiago kuilaza Venezuela kwa mabao 3-1 yaliyofungwa na Alexis Sanchez na Esteban Paredes.


    Katika mchezo mwingine Colombia ikiwa nyumbani imeichapa Ecuador kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na James Rodriguez na Juan Cuadrado.

                                         

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Argentina bila Messi kumbe weupe tu,wanyukwa 2-0 na Bolivia kombe la dunia,Chile,Colombia zashinda Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top