Paul Manjale,Dar Es Salaam.
BAADA ya mapumziko ya wiki mbili kupisha michuano ya kimataifa,ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara maarufu kama VPL inatarajiwa kuendelea tena wikendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja mbalimbali hapa nchini.
Kesho Jumamosi Aprili 01,2017,michezo miwili itachezwa ambapo katika mchezo wa kwanza, mabingwa watetezi wa ligi hiyo,Yanga SC watakuwa wenyeji wa Azam FC kwenye Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam.
Katika mchezo wa pili Wagonga nyundo wa jiji la Mbeya,Mbeya City watakuwa wenyeji wa Ruvu Shooting ya Mlandizi,Pwani.Mchezo huo utachezwa kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Kesho kutwa Jumapili Aprili 02,2017,jumla ya michezo mitano itachezwa.Kagera Sugar itakuwa nyumbani Kaitaba kuwaalika vinara wa ligi hiyo,Simba SC. Majimaji FC watakuwa nyumbani Majimaji,Songea kuwaalika Toto Africans kutoka Mwanza.
Ratiba Kamili
Jumamosi Aprili 01,2017
Yanga SC v Azam FC
Mbeya City v Ruvu Shooting
Jumapili Aprili 02,2017
Kagera Sugar v Simba SC
African Lyon v Stand United
Tanzania Prisons v Mtibwa Sugar
Majimaji FC v Toto Africans
Mwadui FC v JKT Ruvu
0 comments:
Post a Comment