Barcelona,Hispania.
UKISIKIA kuivuruga akili ya mtu mzima,kisha ukamuamuru afanye unavyotaka wewe,basi ndiko huku!!
BARCELONA imeshindwa kabisa kuficha mahaba yake juu ya kiungo mnyumbufu wa Real Madrid,Francisco Román Alarcón Suárez maarufu kama Isco baada ya kuripotiwa kuanza kutumia mbinu kali na chafu kuhakikisha kuwa nyota huyo wa zamani wa Malaga anatua Nou Camp ifikapo mwaka 2018.
Ikijua fika kuwa haiwezi kubisha hodi Real Madrid na kukubaliwa kumnunua Isco kirahisi rahisi, Barcelona imeripotiwa kuwa tayari kumpa Isco kitita cha €20m ikiwa tu atahimili kugomea mkataba mpya Santiago Bernabeu ili iweze kumsajili akiwa mchezaji huru pindi mkataba wake wa sasa utakapokwisha hapo Juni mwakani.
Barcelona imeamua kutumia mbinu hiyo kali na chafu kutokana na ukweli kwamba imekuwa haina mahusiano mazuri na Real Madrid ndani na nje ya uwanja.
Barcelona inamtaka Isco ili kwenda kuchukua nafasi ya kiungo wake mkongwe, Andres Iniesta anayeripotiwa kuwa na mpango wa kutaka kutimka.
0 comments:
Post a Comment