Lima,Peru.
PERU imeweka juu matumaini yake ya kufuzu michuano ijayo ya kombe la dunia baada ya leo asubuhi kuifunga Uruguay mabao 2-1 katika mchezo mkali uliochezwa jijini Lima.
Wageni Uruguay ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza katika dakika ya 30 kupitia kwa Carlos Sanchez.Kuingia kwa bao hilo kuliwaamsha wenyeji Peru ambao walikuja juu na kufanikiwa kupata mabao mawili ya kipindi cha kwanza na cha pili kupitia kwa Paolo Guerrero 35' na Edison Flores 62'.
Ushindi huo wa Peru umechangizwa na Uruguay kucheza pungufu baada ya Jonathan Urretaviscaya aliyekuwa anacheza mchezo wake wa kwanza wa kimataifa kutolewa nje kwa kadi mbili za njano.
0 comments:
Post a Comment