Paul Manjale
KOCHA wa Manchester United,Mreno Jose Mourinho amekiri kuwa kumsajili staa wa Barcelona na Brazil,Neymar ni mziki yaani ni jambo gumu na lisilowezekana kwa sasa.
Mourinho ametoa kauli hiyo leo Alhamisi baada ya hivi karibuni chombo kimoja cha habari cha nchini Hispania kuripoti kuwa wiki iliyopita kocha huyo wa zamani wa Real Madrid alifanya mazungumzo ya siri na Neymar anayedaiwa kuwa na thamani ya £173m.
Mbali ya kukana kuwa habari hizo si za kweli,Mourinho amesema kamwe Barcelona haiwezi kukubali kumwachia mchezaji wake mahiri kama Neymar aondoke kirahisi.
Mourinho amekwenda mbali zaidi hata kufikia kufananisha ugumu wa kumsajili Neymar na ugumu wa kuvunja sefu ya kutunzia fedha ambayo kwa kawaida huwa haivunjiki kirahisi rahisi bila ya kutumia vifaa maalumu vya kuvunjia.
Mourinho amesema siku zote amekuwa akiviomba vilabu anavyovifundisha kumletea wachezaji wanaoweza kupatikana.
Msimu huu Neymar,25,amefunga mabao 14 katika michuano yote,idadi ambayo imedaiwa kuwa ni ndogo zaidi tangu atue Barcelona mwaka 2013-14 akitokea Santos ya Brazil.
0 comments:
Post a Comment