Songea,Tanzania.
TIMU ya Majimaji FC ya mkoani Songea inayoshiriki ligi kuu ya soka ya Vodacom Tanzania bara (VPL) imetangaza kuwasimamisha kwa muda usiojulikana nyota wake wanne kwa utovu wa nidhamu.
Nyota waliokumbwa na balaa la kusimamishwa ni George Mpole,Peter Joseph, Yussuf Mfanyaje pamoja na Ibrahim Tende.
Hata hivyo uongozi wa Majimaji FC haujaweka wazi ni aina gani ya utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na nyota hao tegemeo kubwa kabisa la Wanalizombe.
Wakati huohuo uongozi wa Majimaji FC umesema kuwa umepokea barua za msamaha kutoka kwa wachezaji hao ambazo zitapitiwa na kutolewa maamuzi hivi karibuni.
0 comments:
Post a Comment