728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 31, 2017

    Alexis Sanchez atwaa uchezaji bora wa mwezi Arsenal kwa mara ya tano


    London, England.

    ALEXIS Sanchez ameendelea kujikusanyia tuzo klabuni Arsenal hii ni baada ya Alhamisi usiku kutangazwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Machi.

    Sanchez mwenye umri wa miaka 28 sasa ameibuka mshindi baada ya kupata asilimia 63.3 ya kura zote zilizopigwa na mashabiki wa klabu hiyo.

    Ikumbukwe Machi,Sanchez aliifungia Arsenal mabao mawili kwenye michezo ya kombe la FA na ligi kuu dhidi ya vilabu vya Lincoln City na West Bromwich Albion.Pia alitoa pasi moja ya goli lililofungwa na Danny Welbeck kwenye mchezo dhidi ya Liverpool ulioisha kwa Arsenal kulala kwa goli 3-1.

    Nafasi ya pili imetwaliwa na Theodore Walcott aliyepata kura asilimia 19.9 huku Granit Xhaka akishika nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia asilimia 16.8 ya kura zote.

    Hiyo inakuwa ni tuzo ya tano kutwaliwa na Sanchez msimu huu,mara nyingi zaidi klabuni Arsenal.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Alexis Sanchez atwaa uchezaji bora wa mwezi Arsenal kwa mara ya tano Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top