Paul Manjale.
Cairo,Misri.
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa shirikisho la vyama vya soka barani Afrika (CAF) na mshirika wa karibu wa Rais aliyeng'olewa madarakani, Issa Hayatou,Hicham El Amrani amejiuzulu wadhifa huo.
Katika barua yake aliyoiwasilisha jana Jumapili kwa Rais mpya wa CAF,Ahmad Ahmad,El Amrani, raia wa Morocco,amesema kujiuzulu kwake kunaanzia leo Jumatatu bila ya kutoa sababu ya nini kimefanya achukue uwamuzi huo.
El Amrani,38, amehudumu CAF kwa kipindi cha miaka sita.Aliingia madarakani mwaka 2011 akichukua nafasi ya Mmisri Mustapha Fahmy aliyekwenda kufanya kazi FIFA kama mkurugenzi wa mashindano.
Kabla ya kuukwaa Ukatibu mkuu CAF,El Amrani alikuwa ni meneja masoko wa shirikisho la vyama vya soka barani Asia (AFA).
Amrani na Hayatou wanachunguzwa na CAF baada ya kudaiwa kula rushwa katika kutoa haki za matangazo kwa kampuni ya kurusha matangazo ya Televisheni ya Ufaransa,Lagardere.
0 comments:
Post a Comment