Paul Manjale.
BEKI wa kati wa kimataifa wa Yanga SC,Vincent Bossou amefanya uzembe uliozaa bao moja na kuisababisha timu yake ya taifa ya Togo ikubali kichapo cha mabao 3-0 kutoka kwa Mafarao wa Misri katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Borg El-Arab huko jijini Alexandria.
Bossou alijikuta akiitia matatani Togo katika dakika ya 49 ya mchezo baada ya kuporwa mpira kizembe na Ahmed El-Sheikh aliyeiandikia Misri bao la kuongoza.Bossou alitolewa uwanjani katika dakika ya 56 na nafasi yake kuchukuliwa na Douhadji.
Misri ilijipatia bao lake la pili kupitia kwa Mahmoud Kahraba aliyefunga kwa mkwaju wa faulo katika dakika ya 56'.Bao la tatu limefungwa na kiungo wa Arsenal,Mohamed Elneny katika dakika ya 63' kwa shuti kali la mbali.
Vikosi
Misri:Ekramy,Hegazi,Samir (Tarek 73'),Hafez (Shafy 73'),El Mohamady,Morsy,
Elneny,Kahraba (Gamal 65'),Jakobsen (El Sheikh 46'),Warda (Fathi 61'),Sobhi
Togo:Agblemagnon,Bossou (Douhadji 56'),Dakonam,Ouro-Sama,Kouloun,Lalawelé,Laba (Gbegnon 76'),Gazozo (Boro 74'),Adebayor,Bebou,Yenoussi (Agbegniadan 56')
0 comments:
Post a Comment