728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, March 25, 2017

    Abdi Banda Mchezaji bora mwezi Februari



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Timu ya Simba SC Leo imemtangaza Abdi Banda kuwa mchezaji bora wa mwezi wa pili (February)  akiwashinda wachezaji Laudit Mavugo na Ibrahim Ajibu ambao walikuwa wanafuata Kwa karibu.

    Katika mwezi wa pili Simba walicheza mechi nne na kushinda zote moja ikiwa ya kombe la shirikisho dhidi ya African lyon na tatu za ligi kuu dhidi ya (Majimaji,  Tanzania Prisons na Yanga)  Katika mechi hizo za February mchezaji bora Abdi Banda amecheza mechi mbili dhidi ya African lyon na dhidi ya Yanga Katika mechi hizo Simba ilifungwa goli moja tu na Yanga.  

    Katika Mwezi huo pia wachezaji aliowashida mchezaji bora wa mwezi uliopita Laudit Mavugo alifanikiwa kufunga magoli 4 na kutoa pasi ya goli (assist)  moja Huku Ibrahim Ajibu alifanikiwa kufunga magoli mawili na kutoa pasi mbili za magoli (assist).

    Mchezaji bora wa Simba anapigiwa kura na wanachama na mashabiki wa Simba mwezi wa pili wamemchagua Abdi Banda ambaye atapata tuzo pamoja na fedha Taslimu ya Shilingi laki tano Banda amekuwa akivaa kitambaa cha unahodha Kwa mechi za hiv karibuni.  

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Abdi Banda Mchezaji bora mwezi Februari Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top