728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, March 22, 2017

    Mkizubaa tu Alexandre Lacazette huyo Hispania.

    Madrid,Hispania.

    MKIZUBAA tu imekula kwenu.Hii ndiyo kauli rahisi zaidi unayoweza kuviambia vilabu vya England ambavyo kwa kipindi kirefu vimekuwa vikihusishwa na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji mahiri wa Olympique Lyon,Mfaransa Alexandre Lacazette. 

    Kwa mujibu wa Cadena Cope ni kwamba wagumu wa Vicente Cardeloni,Atletico Madrid tayari wameshafikia makubaliano ya mdomo na  mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kwa ajili ya kumsajili mwishoni mwa msimu huu.

    Taarifa zaidi zimesema Atletico Madrid wamepanga kukamilisha mapema usajili huo iwapo watafikia makubaliano na Olympique Lyon na iwapo wataondolewa adhabu yao ya kutosajili wachezaji wapya baada ya hivi karibuni kufungiwa na Fifa kwa kosa la kufanya udanganyifu kwenye usajili wa wachezaji vijana.

    Ikiwa mpango huo utafanikiwa itakuwa ni habari mbaya kwa vilabu vya Arsenal,Manchester City na Liverpool kwa kipindi kirefu vimekuwa vikimtolea macho mshambuliaji huyo mwenye mabao zaidi ya 20 msimu huu.

    Msimu uliopita Arsenal ilijaribu kutaka kumsajili Lacazette lakini ikakwama baada ya ofa yake ya Euro milioni 35 kukataliwa na Rais wa Jean-Michel Aulas.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mkizubaa tu Alexandre Lacazette huyo Hispania. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top