Buenois Aires,Argentina.
LIONEL Messi yuko kwenye hatari ya kufungiwa mpaka michezo minne ya kimataifa baada ya kutiwa
hatiani kwa kosa la kumtukana matusi ya nguoni mwamuzi msaidizi,Marcelo Van Gasse kwenye mchezo wa wa Alhamisi iliyopita wa kuwania tiketi ya kuwania kufuzu michuano ya kombe la dunia ambapo Argentina ilibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Chile.
Taarifa kutoka mtandao wa Fox Sports Argentina zimesema,Messi,29,mfungaji wa bao pekee la Argentina kwenye mchezo huo anakabiriwa na adhabu ya kufungiwa kati ya michezo miwili mpaka minne kutokana na kosa hilo na huenda adhabu hiyo ikaanzia leo Jumanne kwenye mchezo dhidi ya Bolivia.
Messi alishitakiwa kwenye kamati ya nidhamu ya shirikisho la vyama vya soka vya Amerika Kusini, CONMEBOL baada ya kumtukana,Van
Gasse matusi yasiyoweza kuandikika hapa na kisha kugomea kupeana mikono na mwamuzi huyo mwishoni mwa mchezo huo.
Katika taarifa ya awali iliyowasilishwa baada ya mchezo huo kuisha, haikujumuisha utovu huo wa nidhamu ulioonyeshwa na Messi lakini taarifa ya jana Jumatatu imejumuisha.
Ikiwa Messi atafungiwa kwa idadi yoyote ile ya michezo itakuwa ni pigo kubwa kwa timu ya taifa ya Argentina kwani miamba hiyo ya Amerika Kusini imekuwa ikipata wakati mgumu kupata matokeo mazuri pindi inapocheza bila ya nahodha wake huyo.
0 comments:
Post a Comment