Pichani beki wa Senegal,Lamine Gassama akifanyiwa undava na shabiki
Paul Manjale.
Paris,Ufaransa.
MCHEZO wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa jana Jumatatu usiku kwenye uwanja wa Stade Sebastien Charlety ulioko jijini Paris nchini Ufaransa kati ya miamba wa soka la Afrika,Senegal na Ivory Coast umeshindwa kumalizika katika muda wa kawaida baada ya mashabiki wa timu hizo kuvamia eneo la kuchezea na kuanza kufanya fujo.
Mchezo ukiwa umebakiza dakika mbili kufikia tamati mashabiki waliwazidi nguvu askari waliokuwepo uwanjani hapo na kuingia kwenye eneo la kuchezea na kuanza kufanya fujo mbalimbali ikiwemo kuwakimbiza wachezaji hali iliyomlazimu mwamuzi wa Ufaransa,Tony Chapron kuuvunjilia mbali mchezo huo katika dakika ya 88.
Kabla ya kuvunjika kwa mchezo huo timu hizo zilikuwa tayari zimeshafungana bao 1-1.Sadio Mane alianza kuifungia Senegal bao la kuongoza kwa mkwaju wa penati kabla ya Cyriac Gohi Bi kuifungia Ivory Coast bao la kusawazisha.
0 comments:
Post a Comment