728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, March 23, 2017

    Wabotswana kutua leo tayari kuivaa Taifa Stars



    Dar Es Salaam,Tanzania.

    Timu ya taifa ya Botswana al maarufu kama " the Zebras " yaani pundamilia , wanatarajiwa kutua mchana wa leo jijini Dar Es Salaam kwa ajili ya mchezo wa kujipima nguvu na Taifa Stars hapo jumamosi. 

    Botswana kama ilivyo kwa Tanzania, hawajawahi kushiriki mashindano ya kombe la dunia lakini wamewahi kushiriki mara moja michuano ya mataifa huru ya Afrika ( AFCON ) mwaka 2012 . Tanzania walifanya hivyo mwaka 1980!.

    Botswana wamebatizwa kwa jina la Pundamilia kutokana na wingi wa wanyama pori hao kwenye mbuga zao kama ilivyo kwa twiga Tanzania. Hivyo kama timu ya taifa inasimama vyema kutangaza mali asili za nchi hiyo. 



    Mafanikio ya Botswana kwenye viwango vya FIFA ni mwaka 2010 waliposhika nafasi ya 53! duniani , ubora ambao waliuendeleza vyema na kuwawezesha mwaka 2012 kutinga katika michuano ya AFCON. 

    Kwa sasa Setswana kama wanavyojulikana kwa lugha ya kwao, wapo nafasi ya 116 kisoka duniani wakati wapinzani wao Tanzania wapo nafasi ya 157.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Wabotswana kutua leo tayari kuivaa Taifa Stars Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top