Dar Es Salaam,Tanzania.
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF), limepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha
aliyekuwa Mkurugenzi wake wa Fedha na Utawala, marehemu Edgar Masoud.
Edgar Masoud aliyefariki dunia jana jioni Machi 27, 2017 aliugua ghafla juzi
Jumapili akiwa kanisani kabla ya kukimbizwa Hospitali ya Bochi iliyoko Mbezi
kwa Msuguri ambako alikutwa na mauti akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa familia, Mwili wa marehemu Edgar Masoud unatarajiwa kupumzishwa
kesho Jumatano Machi 29, mwaka huu kwenye makaburi ya Mkuranga mkoani Pwani.
Familia imetoa taarifa kuwa taratibu za mazishi zinafanyika nyumbani kwake
Kimara Kibo jijini Dar es Salaam.
Kwa nafasi ya pekee, katika salamu zake za rambirambi, Rais wa TFF, Jamal
Malinzi alitoa wito kwa ndugu, jamaa, majirani na marafiki kuwa watulivu katika
kipindi hiki kigumu kwa wanafamilia nzima ambao wampoteza mpendwa wao
0 comments:
Post a Comment