James Eduma,Iringa.
Shirikisho la soka nchini TFF limekosoa mpango wa mabingwa wa soka
Tanzania bara Young Africans wa kutaka kuhamisha mchezo wao wa hatua ya mchujo
wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya MC Alger ya Algeria kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.
Afisa habari wa TFF Alfred Lucas amesema mpango huo wa Young
Africans hautowezekana kufuatia uwanja wa CCM Kirumba kutoka CAF ambao ndio
wasimamizi wakuu wa michuano ya klabu bingwa Afrika pamoja na kombe la
shirikisho.
Alfred amesema mchezo wa Young Africans bado utaendelea kuchezwa
jijini Dar es salaam katika uwanja wa Taifa, na kama uongozi wa klabu hiyo
utaendelea na mpango wa kuhamisha mchezo wao dhidi ya MC Alger, wana nafasi ya
kuupeleka Azam Complex ama Aman Zanzibar.
Wakati huo huo shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarifa
za kupangwa kwa tarehe ya mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya Young
Africans dhidi ya Tanzania Prisons wa kombe la shirikisho.
Alfred Lucas amesema taarifa ziliozosambazwa katika mitandao ya
kijamii kuhusu kupangwa kwa tarehe ya mchezo sio za kweli.
Taarifa iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii inaeleza kuwa
mchezo wa Young Africans na Tanzania Prisons wa kombe la shirikisho umepangwa
kuchezwa Aprili 22.
0 comments:
Post a Comment