728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, March 26, 2017

    Burundi yawasili leo tayari kuivaa Stars Jumanne


    Paul Manjale
    Dar Es Salaam,Tanzania.

    TIMU ya taifa ya Burundi maarufu kama Intamba Murugamba imewasili mchana wa leo jijini Dar Es Salaam tayari kuivaa timu ya taifa ya Tanzania,Taifa Stars kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaochezwa Jumanne kwenye Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam.

    Burundi imewasili ikiwa na kikosi cha wachezaji 20 akiwemo mshambuliaji hatari wa Simba SC, Laudit Mavugo na kuweka kambi kwenye hoteli ya De Mag iliyopo Mwananyamala.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Burundi yawasili leo tayari kuivaa Stars Jumanne Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top