728x90 AdSpace

Wednesday, March 22, 2017

Peter Cech aipa pigo Arsenal



London,England.

MAJAALIWA ya Arsenal kushinda vita ya kurejea kwenye nafasi nne za juu (Top Four) yameanza kupata vikwazo baada ya kipa wake namba moja,Petr Cech kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha mwezi mmoja akiuguza jeraha la kigimbi cha mguu.

Cech,34,alipata jeraha hilo Jumamosi iliyopita na kulazimika kutolewa uwanjani na nafasi yake kuchukuliwa na kipa namba mbili,David Ospina katika mchezo ambao Arsenal ilifungwa mabao 3-1 na West Bromwich Albion.




Kufuatia jeraha hilo Cech atakosa michezo minne ya ligi kuu England.Michezo hiyo ni dhidi ya Manchester City,West Ham, Crystal Palace,Middlesbrough pamoja na mchezo wa nusu finali ya kombe la FA dhidi ya Manchester City.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

0 comments:

Post a Comment

Item Reviewed: Peter Cech aipa pigo Arsenal Rating: 5 Reviewed By: Unknown