728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 24, 2017

    Njombe Mji yautaka ubingwa ligi kuu bara

    Njombe,Tanzania.

    KAMA ulidhani Njombe Mji wamepanda ligi kuu bara kuja kushangaa mataa basi andika umeumia.Jamaa wamepania kufanya makubwa msimu ujao ikibidi hata watwae kabisa ubingwa wa ligi hiyo kubwa zaidi nchini.

    Kauli hiyo ya kishujaa na majigambo imetolewa na Mwenyekiti wa timu hiyo,Erasto Mpete wakati akifanya mahojiano na mtandao huu jana Alhamisi.

    Mpete amesema balaa walilolionyesha ligi daraja la kwanza msimu huu lilikuwa trela tu,picha lenyewe litakuwa msimu ujao wa ligi kuu bara ambapo wamepania kuonyesha maajabu kwa kuupeleka ubingwa wa bara mjini Njombe.

    Akiongelea maandalizi ya msimu ujao wa ligi,Mpete amesema Njombe Mji wamepanga kukiongezea nguvu kikosi chao kwa kufanya usajili wa nguvu kwa kusajili wachezaji ndani na wa nje lakini hamu yao kubwa itakuwa ni kusajili wachezaji wazawa ambao wamekuwa na moyo wa kuzipigania timu zao hata pale zinapokuwa hazipo katika hali nzuri kiuchumi.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Njombe Mji yautaka ubingwa ligi kuu bara Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top