728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, March 24, 2017

    Ushindi dhidi ya PSG waiponza Barcelona UEFA

    Barcelona,Hispania.

    UNAUKUMBUKA ule ushindi wa kihistoria wa mabao 6-1 iliyoipata Barcelona hivi karibuni dhidi ya Paris Saint-Germain kwenye hatua ya 16 bora ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya dimbani Camp Nou.

    Basi ushindi huo umeanza kuitokea puani klabu hiyo baada ya jana Alhamisi kulimwa faini ya €19,000 sawa na Milioni 43,700,000 za Tanzania na shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya (UEFA).

    Barcelona imeliwa faini hiyo baada ya kubainika kuwa ilifanya makosa mawili ya utovu wa nidhamu kwenye mchezo huo.

    Kosa la kwanza lilikuwa ni wachezaji na mashabiki wake kuvamia uwanja na kuanza kushangilia ushindi hata kabla mchezo haujaisha.Kosa la pili limetokana na wachezaji watano wa Barcelona kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo huo.Kitendo ambacho kimetafsiriwa kuwa ni utovu mkubwa wa nidhamu kwenye mchezo mmoja.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Ushindi dhidi ya PSG waiponza Barcelona UEFA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top