Krasnodar,Urusi.
WINGA wa Crystal Palace,Wilfried Zaha amefunga bao tamu la kideoni na kuiwezesha timu yake ya taifa ya Ivory Coast kuwafunga wenyeji wa kombe lijalo la dunia,Urusi kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliochezwa huko Krasnodar,Urusi Ijumaa usiku.
Jonathan Kodjia ndiye aliyekuwa wa kwanza kuifungia Ivory Coast bao la kuongoza baada ya mkwaju wake mkali wa dakika ya 30 ya kipindi cha kwanza kwenda moja kwa moja langoni mwa Urusi.
Katika dakika ya 70, Zaha alipachika bao bora kabisa katika mchezo huo na kufanya matokeo yasomeke 2-0.Kabla ya kufunga bao hilo Zaha aliwalamba chenga mabeki watatu wa Urusi na kumfunga kirahisi kipa na nahodha wao mkongwe,Igor Akinfeev.
Pichani Zaha akimtoka mlinzi wa Urusi
Ushindi huo ni wa kwanza kwa Ivory Coast tangu walipotolewa kwa aibu kwenye hatua ya makundi ya michuano ya AFCON iliyofanyika mwanzoni mwa mwaka huu huko Gabon.
0 comments:
Post a Comment