Luxembourg
OLIVIER GIROUD kulia akipongezwa na wachezaji wenzake baada ya kuifungia Ufaransa mabao mawili katika ushindi wa mabao 3-1 ugenini dhidi ya Luxembourg katika mchezo mkali wa kundi A wa kusaka tiketi ya kufunzu michuano ya kombe la dunia la mwaka 2018 huko Urusi.
Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Josy Barthel na kuhudhuriwa na watazamaji 8,000 ilishuhudiwa pia Antoine Griezmann akipata nafasi ya kuifungia bao Ufaransa. Bao la Luxembourg limefungwa na Aurelien Joachim kwa mkwaju wa penati baada ya Blaise Matuidi kumwangusha ndani ya boksi,Daniel Da Mota.
Mchezo mwingine wa kundi A Uholanzi imefungwa mabao 2-0 na Bulgaria kwa mabao ya Spas Delev na kujiweka katika mazingira hatari ya kushindwa kufuzu michuano mikubwa kwa mara ya pili mfululizo.
Kundi B:Cristiano Ronaldo amefunga mabao mawili na kuiongoza Ureno kuifumua Hungary kwa mabao 3-0.Bao jingine limefungwa na Andre Silva.Uswisi imeifunga Latvia bao 1-0 shukrani kwa bao la Josip Drmic.Uswisi iko kileleni mwa kundi B ikiwa na pointi 15 pointi tatu mbele ya Ureno yenye pointi 12.
INGIA HAPA KWA MATOKEO ZAIDI http://www.espnfc.com/world-cup-qualifying-uefa/67/video/3089676/luxembourg-1-3-france
0 comments:
Post a Comment